Lugha Nyingine
Mikoa, Miji na Maeneo 12 ya Magharibi mwa China yatia saini MoU ya Umoja wa Ushirikiano wa Biashara ya Mtandaoni
Viongozi wa Mikoa, Miji na Maeneo 12 ya Magharibi ya China wakitia saini Makubaliano ya Makubaliano ya Maelewano (MoU) ya Umoja wa Ushirikiano wa Biashara ya Mtandaoni. (Picha kwa hisani ya waandalizi wa shughuli)
Shughuli ya kutangaza ushirikiano wa biashara ya mtandaoni (ya kuvuka mipaka) wa China na ASEAN kando ya Njia ya Hariri Mwaka 2024 imefanyika Jumanne, Septemba 24 kwenye Mji wa Nanning katika Mkoa wa Guangxi, China.
Wakati wa shughuli hiyo, mikoa, miji na maeneo 12 ya Magharibi mwa China yalitia saini “Makubaliano ya Maelewano (MoU) ya Umoja wa Ushirikiano wa Biashara ya Mtandaoni wa Mikoa, Miji na Maeneo ya Magharibi mwa China”, na yatafanya mabadilishano na ushirikiano katika biashara ya mtandaoni na upande wa ASEAN na pande nyingine nchini China.
Mwaka 2024 ni mwaka wa kwanza wa muongo wa pili wa ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Ili kuimarisha ushirikiano kati ya mikoa, miji na maeneo ya Magharibi mwa China, Idara ya Biashara ya Guangxi imeanzisha ushirikiano na idara za biasharaza za Sichuan, Shaanxi, Yunnan, Guizhou, Xizang, Chongqing, Mongolia ya Ndani, Gansu, Qinghai, Xinjiang na Ningxia kuunda Umoja wa Ushirikiano wa Biashara ya Mtandaoni.
Makubaliano hayo ya maelewano yataimarisha zaidi mabadilishano na ushirikiano wa biashara ya mtandaoni kando ya Njia ya Hariri, kutumia kikamilifu uwezo wa kufanya biashara na nchi za ASEAN, na kuhamasisha uingiaji wa bidhaa bora za ASEAN kwenye soko la China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma