Lugha Nyingine
OECD yatabiri kuwa uchumi wa dunia utakua kwa kasi mwaka huu na mwaka ujao
Ripoti ya mtazamo wa hali ya uchumi duniani ya muhula wa kati ya mwaka iliyotolewa jana Jumatano na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) imekadiria kuwa, ukuaji wa uchumi wa dunia utatengemaa kwa asilimia 3.2 mwaka 2024 na 2025.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, miongoni mwa nchi za G20, uchumi wa nchi nyingi unaendelea kukua, lakini uchumi wa baadhi ya nchi kama Ujerumani unakua taratibu, huku uchumi wa Marekani unatarajiwa kukua kwa asilimia 2.6 na 1.6 kwa mwaka 2024 na 2025.
Ripoti hiyo inapendekeza kuwa mfumuko wa bei unapoelekea kuwa wa wastani na shinikizo kwenye soko la ajira kupungua, nchi husika zinaweza kufikiria kupunguza viwango vya riba zaidi, lakini zinahitaji kutathmini takwimu kwa wakati halisi na kufanya marekebisho kwa wakati ili kufanya utekelezaji wa sera kwa wakati na mwitikio mwafaka.
Aidha, ripoti hiyo inatoa wito kwa nchi husika kudhibiti ipasavyo matumizi ya fedha na kuongeza mapato ili kuhakikisha uhimilivu wa deni.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma