Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping kutoa heshima kwa mashujaa waliojitolea mihanga kabla ya maadhimisho ya miaka 75 ya Jamhuri ya Watu wa China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 29, 2024
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama cha Kikomunisti cha China na serikali ya China watakwenda kuweka vikapu vya maua kwa kutoa heshima kwa mashujaa waliojitolea mihanga kwenye uwanja wa Tian'anmen katikati mwa Beijing kesho siku ya Jumatatu asubuhi, ambayo ni siku ya kuamkia maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China (PRC).
Viongozi hao watajumuika na wawakilishi kutoka makundi ya sekta mbalimbali katika mji mkuu huo wa China, kuadhimisha Siku ya Mashujaa.
Hafla hiyo ambayo itafanyika mbele ya Mnara wa Mashujaa wa Umma kwenye uwanja wa Tian'anmen itatangazwa moja kwa moja na Kituo Kikuu cha Radio na Televishini cha China.?
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma