Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia alaani dharau ya nchi za Magharibi kwa Umoja wa Mataifa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov akitoa hotuba katika Mjadala Mkuu wa mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 28, 2024. (Xinhua/Li Rui)
UMOJA WA MATAIFA - Nchi za Magharibi zinaendelea kudhoofisha imani ya kimataifa kupitia hatua za upande mmoja zinazokwepa Umoja wa Mataifa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov amesema Jumamosi wakati akihutubia mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Ametoa mfano wa tukio la nchi za Magharibi kudharau Umoja wa Mataifa, akisema kuwa "kila mtu ambaye bado ana hisia za huruma amekasirishwa" kwamba mashambulizi ya kigaidi ya mwaka jana dhidi ya Waisraeli yanatumiwa kuwaadhibu kwa ujumla raia wa Palestina. Ametoa wito wa kukomeshwa mara moja mauaji yao "kwa kutumia silaha za Marekani."
Umoja wa Mataifa unapaswa "kuepuka vishawishi vya kucheza kwenye mikono ya baadhi ya nchi, hasa zile ambazo zinatoa wito wa kutoshirikiana bali kugawanya dunia katika bustani ya maua na msitu -- au kati ya zile zinazoketi kwenye meza ya demokrasia, na zile zilizo kwenye menyu ya chakula," amesema.
"Mapambano na umwamba havitatatua tatizo lolote la kimataifa, vitarudisha nyuma mchakato wa kuundwa kwa utaratibu wa dunia yenye ncha nyingi juu ya msingi wa kuchukuliana kwa usawa ambao utajikita katika haki sawa za nchi kubwa na ndogo," Lavrov amesema.?
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov akitoa hotuba katika Mjadala Mkuu wa mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 28, 2024. (Xinhua/Li Rui)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov akitoa hotuba katika Mjadala Mkuu wa mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 28, 2024. (Xinhua/Li Rui)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma