<sup id="2yyyy"></sup>
  • <sup id="2yyyy"><code id="2yyyy"></code></sup>
  • <sup id="2yyyy"></sup>
    <tr id="2yyyy"><blockquote id="2yyyy"></blockquote></tr>
  • 
    
  • <sup id="2yyyy"><code id="2yyyy"></code></sup>
  • <nav id="2yyyy"><cite id="2yyyy"></cite></nav>
  • <tfoot id="2yyyy"><dd id="2yyyy"></dd></tfoot>
  • 免费a级毛片出奶水在线,18禁无遮拦无码国产在线播放 ,2020国产午夜福利久久,成年女人毛片免费观看中文

    Kutoka takataka hadi utajiri: Soko la kijani la Kenya laongoza kwa udhibiti wa taka

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 15, 2024
    Kutoka takataka hadi utajiri: Soko la kijani la Kenya laongoza kwa udhibiti wa taka
    Samuel Mutua, kaimu meneja wa Kampuni ya Kimataifa ya Biogesi, akiangalia mboga za majani kwenye shamba la kielelezo katika kituo chao cha kuchakata tena taka katika Mji wa Karatina, Kaunti ya Nyeri, Katikati mwa Kenya, Oktoba 9, 2024. (Picha na Robert Manyara/Xinhua)

    NAIROBI - Kwenye soko la Karatina katika Kaunti ya Nyeri, katikati mwa Kenya, Samuel Mutua na timu yake wanaanza kazi zao mapema, wakikusanya na kutenganisha taka kuwa za kioganiki na zisizo za kioganiki.

    Ingawa soko la Karatina limeainishwa kuwa soko la kijani, linazalisha aina zote mbili za taka kutokana na aina mbalimbali za bidhaa zinazouzwa, ikiwa ni pamoja na vifaa vya vifungashio na plastiki. Mutua anakadiria kuwa asilimia 60-70 ya taka sokoni hapo ni za kioganiki.

    Kufikia saa 5 asubuhi, timu hiyo huwa imepakia taka zilizotenganishwa kwenye kigari cha matairi matatu kilichotengenezwa China, kikisafirisha taka zisizoweza kugeuzwa kuwa biogesi hadi kweye dampo la taka huku kikipeleka taka za kioganiki kwenye kituo cha kuchakata tena.

    Utaratibu huu wa kila siku, uliopo kwa miaka miwili iliyopita, umeleta mageuzi katika usimamizi wa taka ngumu katika soko hilo la Karatina.

    Mutua, ambaye ni kaimu meneja wa Kampuni ya Kimataifa ya Biogesi katika kituo hicho cha kuchakata tena taka cha Karatina, ameeleza kuwa taka hizo za kioganiki husindikwa na kuwa mbolea ya mboji na biogesi.

    Kampuni hiyo ya Kenya inabuni teknolojia zenye manufaa kushughulikia changamoto kwa wakulima wa vijijini, huku biogesi ikisaidia kupunguza ukataji miti kwa ajili ya kuni na kupunguza hatari za kiafya kutokana na moshi.

    Kampuni hiyo huuza mbolea ya mboji na mbolea ya kimiminika kwa senti za Kimarekani 38 kwa kilo au lita. Timu hiyo hukuza mboga za majani za kioganiki kama vile sukumawiki na mchicha ikitumia bidhaa hizi kwenye mashamba yao ya kielelezo.

    "Matokeo yake, hatuhitaji mbolea ya sinthetiki ili kukuza mazao yetu kwa sababu mboji ni mbolea ya mchanganyo wa kioganiki," Mutua ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

    Tangu kuanzisha juhudi zao za kuchakata tena taka Mwaka 2022, Mutua na timu yake awali walikusanya tani takriban tatu za taka kila siku -- tani mbili za taka za kioganiki na tani moja ya zisizo za kioganiki. Hata hivyo, kiasi hiki sasa kimepungua na kufikia kati ya tani moja hadi mbili kwani wametoa elimu kwa wafanyabiashara juu ya matumizi mengi ya taka.

    Wafanyabiashara sokoni wameona mabadiliko makubwa ya hali ya sokoni tangu timu hiyo ilipoanza kukusanya taka kila siku. Wakati ambapo taka zilikuwa zikikusanywa mara moja tu kwa wiki, hapo awali, soko mara nyingi lilikuwa ni ngumu kusimamiwa.

    "Walipokuwa wakipakia taka hizo za siku saba kwenye malori, eneo lote lilikuwa limetapakaa taka, na wafanyabiashara na wateja wengi walikwepa soko siku hizo," Esther Nyakio, ambaye ni mfanyabiashara, ameliambia Xinhua. "Sasa, tunafurahi kufanya kazi katika mazingira safi ambayo yanafaa kwa biashara."

    "Lengo letu la baadaye ni kupanua na kuanzisha vituo vya kuchakata tena taka katika kaunti nzima," Mutua amesema.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha

    免费a级毛片出奶水在线
    <sup id="2yyyy"></sup>
  • <sup id="2yyyy"><code id="2yyyy"></code></sup>
  • <sup id="2yyyy"></sup>
    <tr id="2yyyy"><blockquote id="2yyyy"></blockquote></tr>
  • 
    
  • <sup id="2yyyy"><code id="2yyyy"></code></sup>
  • <nav id="2yyyy"><cite id="2yyyy"></cite></nav>
  • <tfoot id="2yyyy"><dd id="2yyyy"></dd></tfoot>